Habari
Je, kusogeza ni kuamini?
Vijana hutumia mifumo ya mitandao jamii zaidi kuliko watu wazima. Lakini wanaiamini kwa kiwango gani?
Shirika la UNICEF pamoja na shirika la Gallup yaliwauliza vijana na watu wazima katika nchi 55 jinsi wanavyoona ulimwengu kwa sasa.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliMifumo ya mitandao jamii ndiyo njia ya kawaida zaidi ambayo vijana hupata habari. Hiyo haimaanishi wanaamini wanachovinjari.
Kwa wastani, ni 23% tu ya vijana wanaosema wanaamini "zaidi" habari za mifumo ya mitandao jamii.
Hiyo ni asilimia ya chini kuliko wanaoamini zaidi vyombo vya habari, wanasayansi na madaktari na watoa huduma ya afya — kwa kila chanzo tulichouliza!
Inabainika kwamba vijana wengi zaidi wanaotumia intaneti duniani ni watumiaji wenye ufahamu wa mitandao jamii.
Ingawa vijana na watu wazima wanaamini vyanzo vya kawaida vya habari...
...imani katika vyanzo hivyo pia ni ya chini sana.
Hatua ya kuchunguza habari kwa undani zaidi inaweza kuwasaidia vijana kutofautisha ukweli na uongo katika enzi hii ya habari za uongo na habari za kupotosha.
Lakini ukosefu wa uaminifu una gharama yake. Ni vigumu kwa vijana kushuku ukweli wa habari wanazozitegemea zaidi.
Ukosefu wa uaminifu pia unadhoofisha umoja wa jamii—na kuchukua hatua ya pamoja ya kutatua matatizo.