Habari
Vyanzo vya kuaminika
Habari zinapatikana kila mahali. Wewe hupataje habari zako?
Shirika la UNICEF pamoja na shirika la Gallup yaliwauliza vijana na watu wazima katika nchi 55 jinsi wanavyoona ulimwengu kwa sasa.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKuna tofauti kubwa zaidi kati ya vijana na watu wazima katika hali yao ya kutegemea vyanzo dijitali dhidi ya vyanzo vya kawaida vya habari.
Pengo hilo ni kubwa kiumri hasa katika matumizi ya mitandao jamii.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliTofauti kubwa zaidi inapatikana katika nchi za mapato ya juu kiasi – ambapo watu wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wana uwezekano mara saba zaidi wa kutegemea mifumo ya mitandao jamii kupata habari kuliko watu wenye umri wa miaka 65 na zaidi.
Katika nchi ambapo kuna ufikiaji mkubwa wa huduma dijitali lakini upatikanaji mdogo wa vyanzo vya kawaida vya habari mtandaoni, mitandao jamii hujaza pengo hilo kwa vijana.
Hali ni tofauti zaidi katika nchi zenye mapato ya chini, ambapo wengi hawawezi kufikia huduma ya intaneti. Karibu asilimia 21 ya vijana katika nchi hizi wanasema hawana kabisa chanzo cha kutegemea kupata habari.