Afya ya Kiakili
Usumbufu wa kiakili
Watu wanahisije nafsini mwao?
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiTuliuliza vijana na watu wenye umri mkubwa kuhusu ustawi wao wa kiakili. Fanya jaribio la maswali ili kuona walivyojibu.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, ni idadi ndogo tu juu ya theluthi moja ya vijana (36%) wanasema huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara.
Hiyo inalinganishwa na 30% kati ya watu wenye umri mkubwa.
Lakini mgawanyiko wa vizazi kuhusu wasiwasi sio sawa katika nchi zote…
Vizazi vya watu wenye umri mdogo vina wasiwasi zaidi ndani ya Marekani…
…Ufaransa…
na Ujerumani.
Wakati vizazi vya watu wenye umri mkubwa vina wasiwasi zaidi ndani ya Lebanoni...
…Ukraine…
na Bangladeshi.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, 19% kati ya vijana wanasema kwamba huwa wanahisi msongo wa mawazo au kuwa na ari ndogo ya kufanya mambo mara kwa mara.
Hiyo inalinganishwa na 15% kati ya vizazi vya watu wenye umri mkubwa.
Usumbufu wa kiakili umeenea zaidi miongoni mwa baadhi ya vijana kuliko wengine.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliVijana walio na umri wa miaka 20-24 wana uwezekano mkubwa wa kuripoti kuwa huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara kuliko wale walio na umri wa miaka 15-19.
Vijana ambao wamemaliza chuo wana uwezekano mdogo wa kuripoti kuhisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi kuliko wale ambao hawajamaliza.
Wale ambao wanasema kwamba huwa wanakumbana na matatizo ya kifedha wana uwezekano mkubwa wa kuripoti kuwa huwa wanahisi dukuduku, kuwa na wahaka au kuwa na wasiwasi mara kwa mara kuliko wale ambao wanasema kwamba wana fedha za kutosha.
Kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu hali ya afya ya kiakili miongoni mwa vijana duniani kote. Ni dhahiri kuwa wasiwasi huo unastahiki kuwepo.