Afya ya Kiakili
Kuwa na mkazo
Kwa kila kizazi, watoto hukabiliwa na nafasi za kipekee za kustawi. Lakini pia wanaweza kuhisi wamelemewa na matarajio.
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiTuliuliza watu kuhusu mkazo ambao unawakumba vijana leo. Unaonaje?
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, 59% kati ya vijana wanaamini kwamba watoto leo hivi hupitia mkazo zaidi wa kufanikiwa kuliko ule ambao wazazi wao walipata walipokuwa watoto.
Hili ni kweli katika takribani nchi zote tulizofanyia utafiti.
Katika 17 kati ya nchi 21, idadi kubwa ya vijana wanaamini kuwa watoto leo hivi hupitia mkazo zaidi wa kufanikiwa.
Lakini sio vijana tu wanaojihurumia…
Idadi kubwa ya watu wenye umri mkubwa kwenye 15 kati ya nchi 21 wanakubali kuwa watoto leo hivi wanakumbana na mkazo zaidi wa kufanikiwa kuliko katika siku zilizopita.