Kuwa na matumaini mema
Mtazamo wa jumla
Je, maisha yetu bora zaidi yamepita au bado yaja? Tazama jinsi maoni yako yanavyolingana na ya watu kote ulimwenguni.
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, watatu kati ya vijana watano wanasema kuwa wanafikiri ulimwengu unaelekea kwa mustakabali bora.
Ingawa matumaini mema ni ya kawaida miongoni mwa vijana, kiwango chake hutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Ni kubwa zaidi ndani ya Indonesia ambapo 82% ya vijana wanaamini kuwa ulimwengu unakuwa mahali bora.
Kwa kulinganisha, ni 29% ya vijana pekee ndani ya Mali walio na mtazamo huu chanya kuhusu ulimwengu wetu.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKatika zote isipokuwa nchi tatu — India, Moroko, na Naijeria — vijana wanaonyesha matumaini mema kuliko watu wenye umri mkubwa.
Katika baadhi ya nchi, pengo kati ya vizazi ni dhahiri kabisa.
Ndani ya Japani vikundi hivyo viwili vya umri vina maoni tofauti sana kuhusu mafanikio ya ulimwengu.
Hili ni kweli katika takribani Marekani…
…na Ajentina.
Kwa jumla, kwa kila mwaka unaoongezeka kwa umri, watu wana uwezekano mdogo kwa 1% kusema kuwa ulimwengu unakuwa mahali bora.
Mambo mengine kando na umri pia huathiri mitazamo ya watu. Watu wanaoripoti kupata matatizo ya kibinafsi ya kifedha wana uwezekano mdogo wa kuwa na matumaini mema kwa ulimwengu. Aidha, wanawake wana uwezekano mdogo kwa 6% kuliko wanaume kusema kuwa ulimwengu unakuwa mahali bora.