Maendeleo ya Utoto
Hatua za utoto
Hamu ya mambo yaliyozoewa inaweza kushurutisha mno. Lakini inapokuja kwa utoto, je, maisha yamebadilika na kuwa bora?
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliIdadi kubwa ya watu wanahisi utoto umeboreka katika nchi nyingi kwenye vipengele vingi katika vizazi vilivyopita.
Katika vipengele hivi tofauti vya utoto, vijana na watu wenye umri mkubwa pia wameshawishika zaidi kuhusu maendeleo katika sehemu za afya…
…na maji safi.
Maendeleo pia yanakiriwa miongoni mwa vizazi — ingawa kwa kiwango kidogo — katika ubora wa kielimu…
…nafasi za kucheza…
…usalama wa kimwili…
…na ufikiaji kwa chakula chenye afya.
Vijana na watu wenye umri mkubwa wana imani ndogo zaidi kwa maendeleo katika ustawi wa kiakili wa watoto.
Mitazamo hii inalingana pakubwa na uhalisia: Katika miongo mitatu iliyopita, ulimwengu umeandikisha maendeleo mazuri mno katika kupanua ufikiaji kwa maji safi, kupunguza utapiamlo miongoni mwa watoto, kutoa huduma muhimu za afya, na mengi zaidi. Mnamo 1990, 9% ya watoto hawakufika siku yao ya kuzaliwa ya tano. Kufikia 2020, idadi hiyo ilikuwa imepungua hadi kufika chini ya 4%
Ingawa watoto wengi sana ulimwenguni kote wanaendelea kutatizika na kunyimwa mahitaji yao ya kimsingi, ni jambo lisilopingika kuwa mafanikio makubwa yametimizwa kwa wengi wa wototo wa ulimwengu.
Kwa jumla, vijana wana uwezekano mkubwa wa kukiri kuboreka kwa maisha ya watoto.
Hilo ni kweli katika takribani nchi zote, lakini hususan ndani ya Ukraine naPeru.
Kwa kulinganisha, vijana hawana uwezekano mkubwa kuliko watu wenye umri mkubwa kuamini kuwa maisha ya watoto yameboreka ndani ya Moroko, India, na Bangladeshi.