Ubaguzi
Usawa kwa baadhi
Misimamo kuhusu haki za watu wa LGBTQ+ imebadilika kwa kasi katika nchi nyingi katika miongo mitatu iliyopita. Lakini ubaguzi unaendelea.
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiIngawa mitazamo kuhusu ubaguzi dhidi ya wanawake na dhidi ya watu wachache kwa kabila, umbari na dini haitofautiani waziwazi kati ya vizazi, inatofautiana inapokuja kwa haki za watu wa LGBTQ+.
Hapa tunaona vijana wakionyesha shauku kubwa zaidi kwa usawa kwa wote kuliko watu wenye umri mkubwa takribani katika nchi zote zilizofanyiwa utafiti - na katika mchakato huo, kusababisha mabadiliko chanya.
Tofauti kubwa za vizazi ni dhahiri katika mataifa mbalimbali…
…kuanzia Japani…
…hadi Uhispania…
…hadi Kenya…
…hadi Peru.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, vijana wa kike wana uwezekano mkubwa kuliko vijana wa kiume kusema kwamba kutowabagua watu wa LGBTQ+ ni muhimu sana kwa takribani pointi asilimia 10.
Kati ya maswali yote katika kura yetu ya maoni, hili linadhihirisha tofauti kubwa zaidi kati ya jinsia miongoni mwa kizazi cha vijana.
Matokeo haya yanafanana na mengine katika utafiti wetu. Kwa jumla vijana wa kike wanaonyesha shauku kubwa zaidi kwa usawa na kupambana na ubaguzi kuliko vijana wa kiume.