Wakala
Uwezo wa mtoto
Watoto wengi hawana haki yao ya kupiga kura. Lakini wanaweza kufanya maoni yao kusikilizwa kwa njia tofauti. Ni nani anasikiliza?
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, idadi kubwa ya vijana wanaamini kuwa ni muhimu sana kwa maoni ya watoto kusikilizwa.
Hilo si jambo la kushangaza. Lakini inaonekana kwamba watu wenye umri mkubwa huwa na mwelekeo wa kukubaliana nao!
Nchi zinazoendelea zina idadi kubwa zaidi ya watu wanaounga mkono viongozi wa kisiasa kuwasikiliza watoto.
Ni jambo la mantiki mno kusikiliza maoni ya watoto katika ulimwengu unaoendelea, ambapo watoto ni fungu kubwa la idadi ya watu.
Katika nchi zenye mapato ya chini na chini ya kati, 48% ya idadi ya watu ni watoto. Kwa wastani, 60% ya watu wenye umri mkubwa wanasema kuwa ni muhimu sana kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto katika nchi hizi.
Kwa kulinganisha, katika nchi zenye mapato ya juu, ni 20% pekee ya idadi ya watu ni watoto. Kwa wastani, 47% ya watu wenye umri mkubwa katika nchi hizi wanasema ni muhimu sana kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto.
Miongoni mwa watu wenye umri mkubwa, tunaona uungaji mkono mkubwa zaidi kwa wanasiasa kuwasikiliza watoto huko Naijeria…
…na Zimbabwe. Katika nchi hizi mbili, nusu ya idadi ya watu ni watoto.