Teknolojia ya Kidijitali
Nafasi za mtandaoni
Ni ulimwengu wa kidijitali. Kizazi chako kimeunganishwa vipi?
Tulifanya utafiti miongoni mwa watu wenye umri wa miaka 15-24 na 40+ katika nchi 21 ili kuchunguza jinsi utoto unavyobadilika.
Soma zaidi kuhusu utafitiJibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliUtafiti wetu ulitambua kuwa kwa wastani, 77% ya vijana huingia mtandaoni kila siku.
Hao ni wengi mno zaidi ya wale walio na umri wa miaka 40+, ambao ni nusu yao tu wanaotumia mtandao kila siku.
Lakini si kila mtu ameunganishwa. Kuna mgawanyiko mkubwa wa kidijitali kote ulimwenguni…
Ndani ya Japani, 96% kati ya vijana huingia mtandaoni kila siku.
Lakini ndani ya Zimbabwe, ni 15% pekee hufanya hivyo.
Zana za kidijitali na huduma za mtandaoni zinaweza kunufaisha watoto kwa njia mbalimbali.
Jibu swali lililo hapa juu ili kujifunza zadi kuhusu hali inayobadilika ya utoto.
Rudi kwenye swaliKwa wastani, idadi kubwa ya vijana wanasema watoto hunufaika sana kutoka kwa kuwa mtandaoni katika sehemu hizi:
Kujuana,
kuwa wabunifu,
…na kujifurahisha.
Zaidi ya yote, vijana wana uwezekano mkubwa wa kuripoti elimu kama faida kubwa ya watoto kuwa mtandaoni.
Watu walio na zaidi ya miaka 40 pia wanasema mtandao unaweza kuwanufaisha watoto sana, lakini wana shauku ndogo kuliko vijana. Hilo ni kweli kuhusu:
Kujuana,
kuwa wabunifu,
kujifurahisha,
na elimu.